Ligi Daraja La Kwanza

Steve Nyerere ahoji wanaochukua fomu

DAR ES SALAAM: Mwigizaji, Steve Mengele maarufu kama Steve Nyerere, ametoa kauli kuhusu wimbi la vijana maarufu kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025.

Kupitia mahojiano maalumu, Steve Nyerere amewataka vijana hao kujiuliza kwa dhati: “Je, wamechukua fomu kwa ajili ya kuwatumikia Watanzania au wanataka kupiga picha bungeni?”

Ameeleza kuwa ni jambo jema kuona vijana wakijitokeza katika siasa, lakini akasisitiza kuwa siasa si jukwaa la kutafuta umaarufu au fursa za binafsi, bali ni wito unaohitaji moyo wa kweli wa huduma kwa wananchi.

“Nafasi ya uongozi si ya kupigia picha bungeni. Ni wajibu, ni dhamana, na ni lazima uwe na moyo wa kweli wa kuwatumikia wananchi,” amesema.

Kauli hiyo imekuja katika kipindi ambacho kumeibuka wimbi la vijana wenye ushawishi mkubwa kwenye mitandao ya kijamii kujitokeza kuchukua fomu ndani ya CCM, hali inayoibua mjadala kuhusu uhalisia wa nia zao katika kugombea nafasi za kisiasa.

Steve amehitimisha kwa kuwasihi vijana hao kufanya tafakuri ya kina kabla ya kuingia kwenye siasa, ili kuhakikisha kuwa wanatoka na nia ya kweli ya kuleta mabadiliko, si kutafuta ‘kiki’.

Related Articles

Back to top button