Serikali yaahidi kuiunga mkono Pazi

Serikali imeahidi kuiunga mkono timu ya mchezo wa kikapu ya Pazi inayokwenda Afrika Kusini kushiriki mashindano ya hatua ya 16 bora kusaka kufuzu fainali za Afrika.
Akizungumza Dar es Salaam leo wakati wa kuiaga timu hiyo Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Damas Ndumbaro amesema serikali itahakikisha timu hiyo inapeperushe vyema bendera ya Taifa wakati wa mashindano hayo.
“Tunaamini Pazi itafanya vizuri, tutawasiliana na Balozi wa Afrika Kusini ili awahimize Watanzania wawape sapoti kwa kipindi chote mtakachokuwa hapo, waiunge mkono timu iweze kufanya vizuri,”amesema Dk Ndumbaro.
Kwa upande wake Kocha Mkuu wa Pazi, Henry Mwinuka amesema timu itaondoka Novemba 18 alfajiri kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya kuianza kampeni ya kutafuta nafasi ya kushiriki fainali za Afrika.