Slot: Tuna jukumu la kushinda taji Anfield

LIVERPOOL:MENEJA wa Liverpool Arne Slot anaamini kikosi chake kina jukumu kubwa la kushinda ubingwa wa ligi hiyo wakiwa katika dimba lao la nyumbani la Anfield watakapotembelewa na vijana wa Ange Postecoglou Tottenham Hostspur jumapili hii.
Liverpool watatangazwa kuwa bingwa wa ligi kuu ya England kwa mara ya 20 ikiwa watashinda mbele ya Tottenham wenye hali mbaya msimu huu huku zikiwa zimesalia mechi 5 kukamilisha msimu huu na point moja pekee kutwaa taji hilo.
Taji la mwisho la Premier League kwa majogoo hao wa jiji katika walilitwaa miaka mitano iliyopita na hali ya hewa ya wakati huo haikuwa rafiki kwakuwa ulikuwa wakati wa Covid-19 na Anfield ilikuwa tupu wakati wakikabidhiwa kombe kwa sababu ya lockdown iliyokuwa ikitekelezwa maeneo mbalimbali duniani.
Liverpool watawatembelea Chelsea katika mchezo wao unaofuata wa ligi kuu baada ya huu wa Tottenham na Slot angependa kuwapa mashabiki wa Liverpool hisia ya kutwaa ubingwa katika dimba la nyumbani
“Ni jukumu zito, tunajua mara ya mwisho klabu hii kutwaa kombe hili kilikua kipindi cha Covid hivyo kila mtu anaikodolea macho jumapili. Tunajua bado kuna kazi ya kufanya tunahitaji hata pointi moja. Mashabiki wetu wanajua vyema hilo, wakija uwanjani inabidi watuunge mkono kwa njia zote wawezazo kama ambavyo wamefanya tangu mwanzo wa msimu”
Liverpool wangewekewa guard of honor na Tottenham jumapili kama Crystal Palace wangefanya ubaya ubwela kwa Arsenal jumatano walipozuru Emirates Stadium na kupata sare ya 2-2.