EPL

Chelsea yaogopa bei ya Osimhen yaendelea na Lukaku

LONDON: CHELSEA imeendelea kushikilia kauli yake ya kwamba mchezaji wa Napoli Victor Osimhen bado ni ghali sana hata baada ya Napoli kupunguza bei ya kumuuza mchezaji huyo.

Klabu hiyo ya Serie A iko tayari kumruhusu Osimhen kuondoka msimu huu wa joto.

Mshambulizi huyo wa Super Eagle ana kipengele cha kuuzwa kwa euro milioni130 sawa na dola za marekani milioni 110.8 katika mkataba wake wa sasa.

Ingawa Osimhen amekuwa akihusishwa na Chelsea, Arsenal na Paris Saint-Germain, hakuna hata mmoja wao ambaye ameonyesha kuwa tayari kukidhi mahitaji ya Napoli.

Hilo limeiacha klabu hiyo ya Italia katika hali mbaya, kwani wanategemea ada ya uhamisho ya Osimhen kufadhili matumizi yao ya majira ya joto, ambayo ni pamoja na dili la Romelu Lukaku.

Ripoti hiyo inadai kuwa wakati wa mazungumzo yao, Napoli walifahamisha kuwa wanaweza kupunguza thamani ya Osimhen hadi €100m (£84.6m).
Hata hivyo, idadi hiyo bado inachukuliwa kuwa kubwa mno na Chelsea, ambao walikuwa wamekubali ada ya pauni milioni 42 na Aston Villa kwa ajili ya mshambuliaji wao wa Colombia Jhon Duran.

Kutokana na dili hilo kutokamilika Napoli wameanza mazungumzo na Chelsea kuhusu mpango wa kumnunua Lukaku staa wa Ubelgiji mwenye thamani ya pauni milioni 38, ambaye wanaona dau lake linawezekana kusajiliwa na timu hiyo.

Kulingana na Corriere dello Sport, Lukaku anataka kuunganishwa tena na Conte huko Napoli na Chelsea sasa watakuwa tayari kupokea ada ya chini kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 ambapo Chelsea wanataka kutoa pauni milioni 25 sawa na dola za marekani milioni 21.1 ili dili hilo likamilike.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button