EPL

Slot: bado ni mapema kuzungumza ubingwa

LIVERPOOL: Bosi wa Liverpool Arne Slot amesema ni mapema sana kwa vinara hao wa Premier League kutajwa kwenye mbio za ubingwa msimu huu baada ya kutanua uongozi wao wa ligi kwa ushindi wa 3-1 dhidi ya Leicester City usiku wa kuamkia leo.

Slot amesema bado kuna michezo 20 na ligi hiyo haitabiriki na lolote linaweza kutokea hivyo kusema moja kwa moja Liverpool ipo kwenye njia ya ubingwa si sawa.

“Kama upo kwenye mpira wa miguu muda mrefu kama mimi na wachezaji, basi mechi 20 kabla ya msimu kuisha hatuzungumzi ubingwa. Kuna changamoto nyingi katikati, majeraha kwa mfano, ni jambo ambalo linaweza ikumba timu yeyote hivyo bado ni mapema mno kuanza sherehe”

“Sidhani kama kuna ushindi mwepesi kwenye michezo iliyobaki. Ingekuwa rahisi kushinda dhidi ya Tottenham lakini tuliruhusu mabao mawili, hii inatuambia ni ngumu kushinda licha ya kuwa na wachezaji wako wote. Hii ndo sababu ni lazima tucheze mchezo mmoja baada ya mwingine msimamo upo upande wetu ndio lakini ni muhimu kuangalia michezo iliyobaki” amesema mholanzi huyo

Liverpool wapo kileleni mwa Premier League na pointi 42, mbele ya Chelsea mwenye point 35 yaani wanaongoza ligi kwa tofauti ya pointi 7 dhidi ya Chelsea walio nafasi ya pili.

Related Articles

Back to top button