Habari Mpya

Singida yatupa dongo zito Yanga

DAR ES SALAAM: BAADA ya kumtambulisha Joseph Guede, Uongozi wa Singida Black Stars wamewatupia dogo Yanga na kuwaambia kuwa wametupa dhababu ambayo wao Swamepata itawasaidia ndani ya timu hiyo kwa msimu wa 2024/25.

Akizungumza na Spotileo, Msemaji wa Singida Black Stars, Hussein Masanza amesema mshambuliaji huyo ataiwasaidia hiyo kwa msimu mpya kwa msimu ujao.

Guede amesaini mktaba wa mwaka mmoja kutumikia timu hiyo yenye maskani yake mkoani Singida akitokea Yanga baada ya mkataba wake wa miezi sita kufikia tamati na kuanza kazi rasmi Singida Black Stars.

“Tumepata mtu, tunaweza kusema hii ni dhahabu hatujamchukuwa kwa mkopo wao, wamemuacha tukamuita mezani na kuzungumza naye, tunaimani kubwa ya kufanya vizuri kwa sababu tumeona uwezo wake kwa kipindi kifupi,” amesema Massanza.

Ameweka wazi kuhusishwa kwa kiungo wa Yanga Jonas Mkude, amesema hana taarifa kamili licha ya jina la mchezaji huyo kujadiliwa katika meza ya kamati ya usajili ya timu hiyo.

“Mkude ni mchezaji mzuri, siwezi kuthibitisha kuwa tupo kwenye mazungumzo na nyota huyo, ninachafahamu kuwa jina lake limekuwa likitajwa sana sasa suala la kusajili lipo katika uongozi wa juu,” amesema ofisa habati wa Singida Black Stars.

Related Articles

Back to top button