Ligi Kuu

Singida Black Stars kama kinyonge hivi..

SINGIDA:KOCHA msaidizi wa Singida Black Stars, Denis Kitambi amesema kuwa kikosi chake kitashuka dimbani kesho dhidi ya KMC FC bila wachezaji Joseph Guede, Edwin John na Jimmyson Mwanuke kutokana na majeraha.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari za michezo kuelekea mchezo huo Kitambi amewataja pia Marouf Tchakei pamoja na Mohamed Kamara ambao bado hawajawasili kambini kwakuwa wapo kwenye majukumu ya timu za taifa.

Amesema licha ya kukosekana kwa wachezaji hao ambao amekiri ni muhimu ndani ya kikosi chake, wamejiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo wa hapo kesho dhidi ya KMC utakaopigwa kwenye Uwanja wa CCM Liti mjini Singida.

Kitambi amesema KMC moja kati ya timu bora za Ligi Kuu Bara ila malengo yao ni kupata matokeo mazuri kwenye uwanja wa nyumbani.

Ligi kuu ya NBC Tanzania Bara inarejea baada ya mapumziko kupisha kalenda ya FIFA –
Imeandaliwa na Brown Juma

Related Articles

Back to top button