Simba yahamishia kambi yake Cairo

CAIRO: KLABU ya Simba imehitimisha sehemu ya kwanza ya kambi yao ya maandalizi mjini Ismailia, Misri, na sasa wamehamia jijini Cairo kuendelea na maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na mashindano ya kimataifa.
Kambi hiyo imekuwa na malengo mahsusi ya kuongeza kiwango cha ufiti wa wachezaji, kujenga umoja wa kikosi na kuandaa mbinu zitakazotumika msimu ujao.
Uhamisho wa kambi kwenda Cairo unalenga kutoa mazingira mapya ya kiufundi na majaribio ya mechi za kirafiki kabla ya kurejea nyumbani Tanzania.
Simba itakaporejea itakutana na tamasha lake maarufu la Simba Day mwezi ujao, ambalo hutumika rasmi kutambulisha wachezaji wapya walioungana na kikosi hicho kwa ajili ya msimu mpya.
Tamasha hilo pia ni fursa ya kuwapa mashabiki burudani na kuwajengea hamasa kuelekea msimu mpya.