Ligi Ya WanawakeNyumbani

Simba Queens ugenini leo

MECHI tatu za raundi ya tano Ligi Kuu ya soka Wanawake Tanzania Bara zinapigwa leo viwanja tofauti.

Bingwa mtetezi Simba Queens ni wageni wa Mkwawa Queens kwenye uwanja wa Chuo Cha Mkwawa mkoani Iringa.

Simba Queens inashika nafasi ya 4 katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 7 baada ya michezo 4 wakati Mkwawa ni ya 9 ikiwa na pointi 1 baada ya michezo 4 pia.

Katika mchezo mwingine Amani Queens itakuwa mwenyeji wa vinara wa ligi hiyo JKT Queens kwenye uwanja wa Ilulu mkoani Lindi.

JKT Queens inaongoza Ligi Kuu ya Wanawake ikiwa na pointi 10 baada ya michezo 4 wakati Amani Queens ipo nafasi ya 7 ikiwa na pointi 4.

Alliance Girls ya Mwanza ipo jijini Dodoma kuwakabili wenyeji wao Fountain Gate Princess kwenye uwanja wa Jamhuri.

Fountain inashika nafasi ya 2 katika msimamo ikiwa na pointi 9 baada ya michezo 4 wakati Alliance ipo nafasi ya 5 ikikusanya pointi 7.

Related Articles

Back to top button