Ligi KuuNyumbani

Simba kuiwinda Singida BS

MENEJA wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema kikosi cha klabu hiyo kitaingia kambini mwishoni mwa wiki kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Singida Big Stars.

Akizungumza na SpotiLeo, Meneja huyo amesema kikosi hicho kinaingia kambini mapema kutokana na uzito wa mchezo.

“Kwa sasa wachezaji wanakuja mazoezini wakitokea majumbani kwao lakini wikiendi hii tutaingia kambini kwa ajili ya mchezo huo ukizingatia pia tutakuwa ugenini kwa hiyo kuna kusafiri na taratibu nyingine, amesema Rweyemamu.

Amesema mpaka sasa wachezaji wote wa Simba wapo katika hali nzuri na wana ari kubwa kuhakikisha wanachukua pointi zote tatu.

Simba na Simgida Big Stars zinatarajiwa kukutana Novemba 9 kwenye uwanja wa Liti mkoani Singida.

Related Articles

Back to top button