FANyumbani

Simba dimbani raundi ya 2 ASFC

MCHEZO kati ya Simba na Eagle zote za Dar es salaam kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa ni miongoni mwa mechi 14 zitakazopigwa leo katika mfululizo wa raundi ya pili Kombe la Shirikisho la Azam(ASFC)-FA.

Kwa mujibu wa ratiba JKT Tanzania itakuwa mwenyeji wa Biashara United kwenye uwanja wa Isamuhyo Dar es Salaam wakati Kengold ni mgeni wa Majimaji kwenye uwanja wa Majimaji, Songea.

Katika michezo mingine Pamba itakuwa ugenini kuivaa Mashujaa kwenye uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma huku Mbao ikiikaribisha Mapinduzi kwenye uwanja wa Nyamagana, Mwanza.

E4M na New Dundee zitaoneshana kazi kwenye uwanja wa Samora wakati African Sports ni mgeni wa Afya kwenye uwanja wa Vwawa, Songwe.

Ratiba hiyo inaonesha pia kuwa Nzega United itakuwa mwenyeji wa KFC kwenye uwanja wa Samora huku Transit Camp ikialikwa na matajairi wa dhahabu Geita Gold kwenye uwanja wa Nyankumbu, Geita.

Mtama Boys itakuwa ugenini kupambana na wanambogomaji, Ihefu kwenye uwanja wa Highland Estates, Mbeya wakati Kagera Sugar ni wenyeji wa Buhare kwenye uwanja wa Kaitaba, Kagera.

Katika mechi nyingine walima zabibu Dodoma Jiji itaikaribisha TMA Stars kwenye uwanja Jamhuri huku wanakuchele Ndanda ikiwa mgeni wa maafande wa Ruvu Shooting kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Nao uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga utawaka moto wakati wgosi wa kaya, Coastal Union itakapoikaribisha Tanga Middle.

Matokeo ya michezo mingine iliyopigwa Desemba 9 ni kama ifuatavyo:

Fountain Gate   1 – 1   Rhino Rangers
(pen 7- 8)
Ndunguti Stars  1 – 3  Gwambina
African Lyon      2 – 2  Mbuni
(pen 1 -3)

Polisi Katavi      1 -1   Mbeya Road
(pen 3 -1)
Green Warriors  0 -0   Stand United
(pen 4-2 )
Mbeya City        5- 1    Stand
Azam               9 – 0    Malimao

Related Articles

Back to top button