Kwingineko

Simanzi, Diogo Jota wa Liverpool afariki ajalini

ZAMORA: Mshambuliaji wa mabingwa wa soka la Engalnd Liverpool FC Diogo Jota amefariki dunia katika ajali ya gari iliotokea katika jimbo la Zamora lililo kaskazini Magharibi mwa Hispania siku chache tu baada ya harusi yake.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno alikuwa na umri wa miaka 28 pamoja na timu ya Liverpool Jota aliwahi kuichezea Wolverhamption Wanderers ya Ligi Kuu ya England.

Akiwa Liverpool Jota alicheza mechi 123 akifunga mabao 47 kati ya msimu wa mwaka 2020 na na msimu uliomalizika wa 2024/2025.

Mshambuliaji huyo pia alikuwa sehemu ya kikosi cha Ureno kilichotwaa ubingwa wa UEFA Nations League mwezi uliopita

Juni 22, 2025 Jota na mpenzi wake wa muda mrefu Rute Cardoso walifunga ndoa ya kanisani jijini Porto nchini Spain na alikuwa amechapisha picha za harusi kwenye instagram, akisema ‘Yes to forever’.

Ajali hiyo pia imechukua uhai wa mdogo wake André Silva ambaye pia ni mwanasoka aliyekuwa akiitumikia klabu ya FC Penafiel ya Portugal inayoshiriki Ligi Daraja la pili nchini humo.

Related Articles

Back to top button