Kwingineko

Kubadilishana jezi kwamponza Kylian Mbappe

MUNICH: BAADA ya timu ya taifa la Ufaransa kuondoshwa hatua ya nusu fainali kwa kipigo cha timu yao cha mabao 2-1 dhidi ya timu ya taifa la Hispania mashabiki wat imu hiyo wamemtupia maneno ya kashfa na wamemzomea nahodha wao Kylian Mbappe wakidai hakupaswa kubadilishana jezi na mchezaji wat imu pinzani kabla ya mechi kuisha.

Mbape alibadilishana jezi na mchezaji wa Hispania wakati wa mapumziko ya mchezo huo wa nusu fainali ya Euro 2024.

Katika mchezo huo Mbappe alitoa pasi ya bao la kwanza la dakika ya nane ya mechi hiyo iliyopigwa mjini Munich wakati krosi yake ilipopigwa kwa kichwa na Randal Kolo Muani, lakini Uhispania ikasawazisha kupitia kwa mshambuliaji wa miaka 16, Yamine Lamal na Dani Olmo akafunga bao la pili na la ushindi wa 2-1 hadi mapumziko.

Picha zinamuonyesha Mbappe akipanda ngazi kuelekea vyumba vya kubadilishaia nguo akiwa ameshikilia jezi ya Uhispania mashabiki walibaki wakimshangaa mshambuliaji huyo.

Mashabiki wengine waliendelea kuandika katika page zao za X wakimtuhumu mshambuliaji huyo kwa kubadilishana jezi kabla ya mchezo kuisha tuhuma nyingi zilimweleza Mbappe kutokuwa makini na jambo hilo ambalo kwake aliliona la kawaida lakini mashabiki wengine walilihusisha na Imani za kishirikina.

Related Articles

Back to top button