FA

“Sikupenda matuta” – Eng. Hersi

ZANZIBAR. RAIS wa klabu ya Yanga, Hersi Said amesema hakupenda kuona fainali ya kombe la Shirikisho la CRDB Bank kwenda kwenye mikwaju ya penalti kwa sababu hawana bahati na upigaji wa penalti

Akizungumza na Spotileo, Hersi Saidi amesema alikuwa na wasiwasi na hakupenda kufikia hatua ya kupiga mikwaju ya penalti kwa sababu ya kumbukumbu za kupoteza michezo miwili kwa staili hiyo.

“Nilitamani mpira umalizike ndani ya dakika 90, kwa kuwa michezo miwili tumeondolewa katika hatua ya penalti, Ngao ya Jamii dhidi ya Simba na hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Mamelodi Sundowns,” amesema Hersi.

Ameongeza kwa kulingana na ubora wa Azam FC walionyesha kwa msimu huu hawakutaka kufika katika hatua ya kupiga mikwaju ya penalti na kuomba mechi itamatike ndani ya dakika 90.

“Tumecheza fainali nyingi lakini hii ina ubora mkubwa na hutokana na ubora wa timu zote mbili, Azam FC walikuwa bora sana lakini kama ninavyosema suala la penalti haina mwenyewe.

Nimpongeze sana kipa wa Azam Fc (Mohammed Mustafa), alikuwa bora sana hasa kuokoa mipira mingi ya hatari lakini Diarra (Djigui) naye amefanya kazi kubwa hasa kucheza penalti ya mwisho ambayo muhimu kwetu kutangaza ubingwa wa mara mbili mfululizo,” anasema Hersi.

Ameeleza kuwa sasa wanaenda kujipanga kwa ajili ya msimu ujao ikiwemo kuboresha kikosi cha timu kufanya usajili mzuri kwa kuongeza baadhi ya wachezaji ili msimu ujao kurejesha kombe la Ngao ya Jamii ambalo wamelipoteza msimu wa 2023/24

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button