EuropaKwingineko

Sevilla vs Roma: Fainali ya kibabe Europa

MIONGO miwili imepita tangu Jose Mourinho aliposhinda taji la kwanza la ulaya akiingoza Porto kutwaa kombe la UEFA mwaka 2003.

Baada ya miaka 20 sasa mreno huyo anaweza kunyakua taji la sita la ulaya wakati klabu yake ya Roma itakapoikabili Sevilla katika fainali ya Kombe la Europa jijini Budapest, Hungary.

Rekodi ya Mourinho katika fainali zilizopita ni kwamba ameshiriki tano na ameshinda tano.

Sevilla imeshinda mara sita katika michuano hiyo mara nyingi kuliko klabu nyingine yoyote.

Klabu hiyo pia imekuwa na bora inapofika fainali. Tangu 2006 imechza fainali mara sita imeshinda mara sita.

“Sifikirii sana kuhusu kilichotokea kabla. Historia haishindi mechi. Ni fainali mpya. Ni historia mpya,” amesema Mourinho.

Kuingia fainali Sevilla imeifungasha virago Juventus wakati Roma imeitoa Bayer Leverkusen.

 

Related Articles

Back to top button