Mitindo
Serikali yaombwa ‘kuitupia jicho’ mitindo

DAR ES SALAAM: SERIKALI imetakiwa kulitupia jicho sekta ya mitindo nchini kwa kuipa kipaumbele na sapoti sawa na inavyofanya kwenye sekta ya michezo, hasa kwa wachezaji wa mpira wanapofunga magoli.
Akizungumza na HabariLeo, Msemaji wa Tanzania Fashion Festival (TAFF), Bhoke Egina, alisema lengo ni kuona sekta ya ubunifu inapata mashindano, pongezi na umaarufu sawa na ule wa michezo ili kukuza ajira na ubunifu wa vijana.
“Tunataka ushindani uliopo kwenye mpira uingie pia kwenye sekta ya ubunifu. Jukwaa la mitindo liwe kubwa zaidi, na wabunifu wetu washiriki kwenye matamasha makubwa duniani kama Marekani, Ufaransa na nchi zingine zilizoendelea,” amesema Bhoke.