Tennis

Serena Williams akana kurudi kwenye tenisi

NEWYORK: WIKI hii, kulizuka tetesi kubwa kuhusu mcheza tenesi maarufu duniani Serena Williams kurejea kwenye ulingo wa tenisi, baada ya jina lake kuonekana kwenye orodha ya wachezaji waliojisajili kwa ajili ya vipimo vya doping na Taasisi ya Uadilifu wa Tenisi (ITIA).

Miaka mitatu sasa tangu alipoacha mchezo huo rasmi, baada ya kufanya safari ndefu ambayo ilimfanya kuwa mmoja wa wachezaji bora zaidi katika historia ya tenisi, akishinda mashindano 23 ya Grand Slam.

Serena, mwenye umri wa miaka 44, hakuwahi kushiriki mashindano makubwa ya tenisi tangu US Open ya 2022, ambapo alitangaza kujitenga na mchezo huo ili kuzingatia familia yake. Hata hivyo, uvumi ulianzishwa baada ya ITIA kutangaza kwamba jina lake liko kwenye orodha ya wachezaji waliowekwa kwenye orodha ya vipimo vya doping.

Serena alitumia mitandao yake ya kijamii, hasa jukwaa la X zamani Twitter, kubainisha wazi kuwa hana mpango wa kurudi tena kwenye mchezo wa tenisi. Aliandika, “Omg y’all I’m NOT coming back. This wildfire is crazy,” akionyesha bila shaka kuwa hana nia ya kurudi tena kwenye ulingo wa tenisi baada ya kustaafu mwaka 2022.

Orodha ya ITIA kwa vipimo vya doping ni muhimu kwa wachezaji wanaotaka kushiriki mashindano rasmi ya tenisi yanayoidhinishwa. Mashindano haya yanahitaji kuwa na wachezaji waliokuwa kwenye orodha ya vipimo kwa angalau miezi sita kabla ya mashindano, na vipimo vya nje ya mashindano vinawezesha mamlaka ya tenisi kufanya ukaguzi wa doping hata wakati wa kipindi cha kupumzika kwa wachezaji.

Serena amekuwa akiishi maisha ya faraja na familia yake ndogo, pamoja na mjasiriamali wa teknolojia, Alexis Ohanian, na wanaye wawili wa kike. Pamoja na kuonekana mara kwa mara kwenye matukio ya umma, hivi karibuni alitokea kwenye tamasha maarufu la Super Bowl mwaka 2025 akiwa na msanii Kendrick Lamar.

Related Articles

Back to top button