Semenyo atua Man City

MANCHESTER:KLABU ya Manchester City imefanikiwa kumsajili mshambuliaji wa Ghana, Antoine Semenyo, kutoka Bournemouth ili kuongeza nguvu kwenye safu yao ya ushambuliaji kabla ya msimu wa EPL na UCL kumalizika.City imemsajili mchezaji huyo kwa mkataba wa miaka mitano na nusu na atavaa jezi namba 42, namba iliyowahi kuvaliwa na mkongwe Yaya Toure.

Semenyo, mwenye umri wa 26, tayari ana mabao 10 msimu huu na anatajwa kuwa miongoni mwa washambuliaji bora Ligi Kuu England. Ni sajili ya kwanza ya City katika dirisha la Januari,akiwa amenaswa kwa kiasi kinachoripotiwa kuwa pauni milioni 65 sawa na dola za kimarekani milioni 87.
Mshambuliaji huyu anayeweza kucheza kwenye pande zote mbili za winga, amesema: “Nimekuwa nikiifuatilia City kwa muongo mmoja uliopita chini ya Pep Guardiola, na wamekuwa timu ya nguvu kwenye EPL na pia wanafanya vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa,Kombe la FA na Kombe la Ligi. Kuwa hapa ni heshima kubwa kwangu na najua hatma yangu itakuwa bora zaidi huko mbele.”
Semenyo ataingia kikosini kupambania nafasi na wachezaji wengine wa pembeni kama Jeremy Doku, Rayan Cherki, Phil Foden, Omar Marmoush, Savinho na Oscar Bobb




