Kuogelea

Romeo Mihaly atinga fainali kuogelea Afrika

MCHEZAJI wa timu ya taifa ya kuogelea Romeo Mihaly ametinga hatua ya fainali michuano ya kuogelea ya vijana ya Afrika inayofanyika nchini Misri.

Kwa mujibu wa taarifa ya Msemaji wa Chama cha Kuogelea Tanzania (TSA) Sebastian Kolowa, Romeo aliogelea mbio mbili, mita 100 backstroke na mita 100 breaststroke na amefanikiwa kuingia fainali katika mbio za mita 100 backstroke.

“Tunawashukuru kwa kuendelea kufuatilia taarifa kutoka kwa timu ya Tanzania kwenye mashindano ya vijana ya Afrika yanayoendelea Misri, Romeo amefika amejitahidi amefika fainali,”amesema.

Kwa upande wa Christian Fernandes aliogelea mita 100 breaststroke na mita 50 butterfly na amefanikiwa kuweka rekodi mpya za kibinafsi katika mbio zote mbili.

Naye Bridget Heep aliogelea mita 50 breaststroke na amefanikiwa kuweka rekodi mpya ya kibinafsi.
Aminaz Kachra walishiriki katika mbio za mita 100 backstroke na wote wawili wamefanya vizuri katika mashindano yao.

Kolowa amesema licha ya hali ya hewa ambayo sio nzuri jijini Cairo, timu inaendelea vyema na morali iko juu.

Related Articles

Back to top button