Familia

Rihanna aomboleza kifo cha baba yake

CALIFORNIA: BABA wa Mwanamuziki Rihanna Fenty, Robyn Fenty amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 70 kutokana na kuugua kwa muda mfupi.

Kwa mujibu wa Mtandao wa Starcom uliripoti kwamba Ronald Fenty amefariki dunia kutokan an kuugua kwa muda mfupi.

Chombo hicho kiliripoti kwamba wanafamilia akiwemo Rihanna aliyewahi kutamba na wimbo wa ‘Umbrella’ wamekusanyika huko California, ambapo Fenty aliaga dunia mapema asubuhi, lakini hakukuwa na maelezo yoyote kuhusu msiba huo.

Jarida la PEOPLE baadaye lilithibitisha habari hiyo, ingawa sababu rasmi na tarehe ya kifo bado haijawekwa wazi.

Habari hizi zinakuja siku chache baada ya TMZ kuripoti kuwa kaka wa Rihanna, Rajad Fenty ameonekana katika Kituo cha Matibabu cha Cedars-Sinai huko Los Angeles, na kudai kuwa hitmaker huyo wa ‘Umbrella’ pia alikuwa naye.

Ronald waliachana na mama wa Rihanna, Monica Braithwaite mwaka 2002 akiwa na binti zake Kandi miaka 54 na Samantha Fenty miaka 44, pamoja na mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 35 Rorrey Fenty.

Kabla ya talaka yao, Ronald na Monica walikuwa wamelea watoto wao huko Bridgetown, Barbados ambako alifanya kazi kama msimamizi wa ghala yeye akiwa mhasibu.

Rihanna alikuwa na uhusiano mbaya na babake alipokuwa akikua na alikuwa katikati ya vita vya hadharani naye baada ya kuzungumza na waandishi wa habari vibaya aliposhambuliwa na mpenzi wake Chris Brown mwaka 2009.

Hata hivyo, katika miaka iliyofuata, walipatana, lakini mwaka wa 2019, Rihanna alimshtaki babake kwa madai ya kutumia jina lake vibaya ili kujinufaisha kifedha lakini akachagua kutupilia mbali malalamiko hayo wiki chache kabla ya kupelekwa kortini.

Rihana kwa sasa anatarajia mtoto wa tatu na rapa A$AP Rocky ambaye tayari wana Rza, wawili, pamoja na Riot mwenye umri wa miezi 22 na Ron hapo awali alishiriki jinsi alivyoidhinisha uhusiano wa binti yake.

Related Articles

Back to top button