EPL

Rice:Tungeweza kuwapiga 10

LONDON: DECLAN Rice anaamini Arsenal walipaswa kuwapa Tottenham kipigo cha kihistoria kutokana na nafasi nyingi walizotengeneza kwenye mechi yao ya North London Derby.

Arsenal walishinda 2-1, ushindi muhimu uliowakaribia pointi nne nyuma ya viongozi wa ligi, Liverpool. Hata hivyo, timu ya Mikel Arteta ilikosa nafasi nyingi, licha ya mashambulizi makali na kupiga mashuti 14.

Rice alisema: “Tulitawala mchezo, hasa dakika 45 za kwanza. Tulistahili kufunga mabao 10. Kukosa nafasi nyingi ni jambo la kuvunja moyo.”

Arsenal walikosa makali mbele ya lango, huku Raheem Sterling, aliyepangwa badala ya Gabriel Martinelli, akishindwa kuwashawishi. Pia, timu inakabiliana na majeraha ya muda mrefu ya wachezaji muhimu kama Gabriel Jesus, Bukayo Saka, na Ethan Nwaneri.

Kabla ya mechi, wachezaji wa Arsenal walimuenzi Jesus kwa kuvaa jezi zenye jina lake.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button