RASMI: Benzema kuondoka Madrid

KARIM Benzema anaondoka Real Madrid mwishoni mwa msimu huu, baada ya miaka 14. Timu hiyo imethibitisha.
Mfaransa huyo alijiunga na Real akitokea klabu ya Lyon mwaka 2009 na amecheza mechi 657, akifunga mabao 353 – amecheza mechi 42 katika mashindano yote hadi sasa, akifunga mabao 30 na kusaidia wengine sita msimu huu.
Hakucheza katika ushindi wa 2-1 wa Real dhidi ya Sevilla Mei 27, lakini huenda akacheza kwa mara ya mwisho katika mechi yao ya mwisho ya ligi msimu huu dhidi ya Athletic Bilbao leo usiku.
Benzema, 35, alishinda LaLiga mara nne na kunyanyua Ligi ya Mabingwa mara tano.
Taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti rasmi ya klabu iliyotafsiriwa kutoka Kihispania – inasomeka: “Real Madrid CF na nahodha wetu Karim Benzema wamekubali kumaliza kipindi chake kizuri na kisichosahaulika kama mchezaji wa klabu yetu.
Jana kocha wa Madrid, Carlo Ancellotti alithibitisha kuwa na uhitaji wa mchezaji huyo na kujipa matumaini ya kubaki naye klabuni hapo.