Tetesi

Ramsdale kuondoka Arsenal

TETESI za usajili zinaeleza kuwa Arsenal inakusudia kumruhusu golikipa Aaron Ramsdale kuondoka klabu hiyo mwisho wa msimu lakini haitamruhusu aondoke wakati wa dirisha la uhamisho Januari 2024.(90min)

Kiungo wa kidachi Donny van de Beek anasema ataomba kuondoka Manchester United Januari, 2024 iwapo hataanza kucheza mechi nyingi zaidi.
(Diario AS, via Sky Sports)

Tottenham Hotspur ipo tayari kushindana na Manchester United na Liverpool kuwania saini ya beki wa kifaransa wa klabu ya Nice, Clair Todibo mwenye umri wa miaka 23.(Evening Standard)

PSG inatarajiwa kuanza mazungumzo ya kumsajili kiungo wa Corinthians anayeng’ara kwa sasa, Gabriel Moscardo. (Fabrizio Romano)

Related Articles

Back to top button