Tetesi
Palhinha mambo safi Bayern Munich

KIUNGO wa Ureno, Joao Palhinha leo atakamilisha uhamisho wake kunako Bayern Munich.
Taarifa ya mwandishi wa habari za michezo nchini Italia, Fabrizio Romano imeeleza kuwa Palhinha atasaini mkataba wa miaka minne utakaomuweka klabuni hapo hadi 2028.
Wiki iliyopita Palhinha alikamilisha vipimo vya afya.
Fulham itapokea €50m. Romano amesema Bayern itamtangaza Palhinha, Olise kisha timu hiyo itaendelea na uhamisho wa Jonathan Tah.
Palhinha alijiunga na Fulham akitokea Sporting CP ya Ureno baada ya kuitumikia Braga na Belenenses za nchini humo kwa mkopo.
Usajili wa kiungo huyo utakuwa wa pili baada ya Michael Olise wiki iliyopita kutua jiji la Munich kukamilisha usajili wake.