Africa
Raja vs Simba saa 7 usiku
MCHEZO wa marudiano Ligi ya Mabingwa Afrika kundi C kati ya Raja Casablanca ya Morocco na Simba utapigwa saa 7 usiku Aprili 1.
Mechi hiyo itafanyika uwanja wa Mohammed V jijini Casablanca na itakuwa leo saa 4 usiku kwa saa za Morocco.
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Dar es Salaam Simba ilikubali kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Raja.
Michezo mingine ya Ligi ya Mabingwa Afrika leo ni kama ifuatavyo:
Kundi C
Horoya vs Vipers
Kundi D
Zamalek vs Al-Merreikh




