Tetesi

PSG yataka watano Real kulipiza kisasi

TIMU ya Paris Saint-Germain imeripotiwa kuandaa orodha ya wachezaji wa Real Madrid ‘Los Blancos’ ili kuwasajili kulipiza kisasi cha klabu hiyo ya Hispania kila mara kuonesha nia kwa Kylian Mbappe.

Nia inayoendelea ya Real Madrid kwa nyota huyo wa Ufaransa imeleta misukosuko kwa mabingwa hao wa Ligue 1, ambaye anaonekana anakusudia kwenda Bernabeu majira yajayo ya kiangazi.

Kwa mujibu wa tovuti ya michezo, Sport, sasa PSG inapanga kuvamia vito vya Madrid kujibu mashambulizi, huku Rais wa PSG Nasser Al-Khelaifi akionekana ana nia kusajili wachezaji watano.

Wachezaji hao ni Vinicius Jr, Rodrygo, Aurelien Tchouameni, Eduardo Camavinga na Federico Valverde.

Kikwazo kikubwa katika mpango huo ni vifungu vikubwa vya kuachiwa ambavyo klabu za Hispania zimekuwa zikiwawekea wachezaji wao wenye vipaji.

Vinicius Jr ameripotiwa kusaini mkataba mpya majira ya kiangazi wenye kifungu cha kuachiwa cha pauni milioni 860 sawa na shilingi trilioni 2.6 na Madrid mara chache hupoteza wachezaji wenye vipaji kwenda klabu nyingine.

Related Articles

Back to top button