Ligi KuuNyumbani

Prisons vs Polisi dabi ya kijeshi

Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara inaendelea leo kwa michezo mitatu kupigwa Mbeya, Singida na Lindi.

Katika uwanja wa Sokaine jijini Mbeya timu mbili za jeshi zitaumana, Polisi Tanzania ikiwa mwenyeji wa Tanzania Prisons.

Tanzania Prisons ipo nafasi ya 11 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 9 baada ya michezo 7 wakati Polisi Tanzania inashika nafasi ya 15 ikiwa na pointi 5 baada ya michezo 8.

Mchezo mwingine ni kati ya Dodoma Jiji na Mtibwa Sugar katika uwanja wa Liti mkoani Singida.

Mtibwa Sugar inashika nafasi ya 5 ikiwa na pointi 12 baada ya michezo 8 wakati Dodoma Jiji ni ya mwisho nafasi ya 16 ikiwa na pointi 5 baada ya michezo 7.

Nayo Namungo baada ya kupoteza michezo miwili mfululizo ugenini itakuwa mwenyeji wa Kagera Sugar katika uwanja wa Majaliwa mkoani Lindi.

Namungo ipo nafasi ya 7 ikiwa na pointi 11 baada ya michezo 7 wakati Kagera Sugar 13 ikiwa na pointi 8 baada ya michezo 8.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button