
NYASI za uwanja wa Sokoine jijini Mbeya leo zitawaka moto wakati Tanzania Prisons itakapoikaribisha Azam katika mchezo wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara.
Azam ipo nafasi ya 5 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 8 baada ya michezo 4 wakati Prisons inashika nafasi ya 11 ikiwa na pointi 4 baada ya michezo 4 pia.
Mara ya mwisho timu hizo kukutana katika mchezo wa ligi kuu Juni 22, 2022 Azam iliifunga Prisons bao 1-0.
Azam na Tanzania Prisons zimekutana mara 13 huku Prisons ikiambulia ushindi mara 1 wakati Azam imeshinda mara 9 na michezo 3 zimetoka sare.
Katika mfululizo wa ligi hiyo Septemba 29 Ruvu Shooting ilitumia vizuri uwanja wa nyumbani baada ya kuichapa Coastal Union mabao 2-1 katika uwanja wa Uhuru.
Nayo Dodoma Jiji ikapata ushindi wa kwanza katika ligi baada ya kutoka kufua mbele dhidi ya Geita Gold kwa bao 1-0 katika uwanja wa Liti mjini Singida.