
MICHEZO mitatu ya mzunguko wa 19 ya Ligi Kuu Tanzania Bara inapigwa leo viwanja tofauti huku mechi kati ya Simba na Tanzania Prisons ikiwa kivutio.
Wekundi wa Msimbazi, Simba inaikaribisha Prisons kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa,Dar es Salaam katika mechi inayotarajiwa kuwa ya ushindani.
Wadhamini wa Prisons, Silent Ocean wameahidi kutoa sh milioni 30 iwapo timu hiyo itaifunga Simba na sh milioni 10 ikipata sare katika mchezo huo.
Simba inashika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 41 wakati Prisons ipo nafasi ya 11 ikiwa na pointi 21.
Kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma walima miwa Kagera Sugar itakuwa wageni wa walima zababi Dodoma Jiji.
Kagera Sugar ipo nafasi ya 6 ikikusanya pointi 24 wakati Dodoma Jiji inashika nafasi ya 12 ikiwa na pointi 18.
Nayo Singida Big Stars itakuwa mwenye wa Geita Gold kwenye uwanja wa CCM Liti mjini Singida.
Singida BS inayoshika nafasi ya 4 ina pointi 34 wakati Geita Gold ipo nafasi ya 7 ikiwa na pointi 24.