BurudaniMuziki

Priscilla Ojo afurahia ukaribu wa mtoto wake na wa Mohbad

LAGOS: MUIGIZAJI maarufu wa filamu za Nollywood na Mitandaoni, Priscilla Ojo, amegusa mioyo ya wengi mtandaoni baada ya kushiriki video na picha za kupendeza zikimuonesha Liam, mtoto wa marehemu mwimbaji Mohbad, akifurahia muda mzuri pamoja na mtoto wake mchanga, Rakeem.

Tangu kifo cha Mohbad, ambaye ni mjane wake Wunmi na mwanawe Liam wamekuwa karibu sana na familia ya Iyabo Ojo, mama yake Priscilla uhusiano uliodumu na kuimarika zaidi baada ya Iyabo kujitolea kupigania haki ya marehemu msanii huyo.

Kwa muda sasa, familia ya Ojo imekuwa ikimchukulia Liam kama sehemu ya familia yao, jambo linaloonekana wazi kuwa alikuwa mtu wa karibu mno na familia hiyo.

Kupitia mtandao wake wa Snapchat, Priscilla alitoa taarifa ya kupendeza kuhusu Liam, akifichua jinsi mtoto huyo mdogo anavyoonesha upendo na uangalizi wa kindugu kwa Rakeem.

Alisema awali Liam alionekana kuwa na wivu kidogo, lakini baadaye wakawa marafiki wakubwa na kuanza kucheza pamoja kwa furaha jambo lililoonesha ukaribu wa dhati kati ya familia hizo mbili.

Cha kuvutia zaidi, Liam pia alikuwa bwana harusi mdogo katika sherehe ya harusi ya Priscilla, akiwavutia wageni wote kwa tabasamu lake na furaha ya mtoto asiye na hila.

Mashabiki mtandaoni hawakuweza kujizuia kufurahia ukaribu huo, wakimsifia Priscilla na mama yake Iyabo kwa kuendelea kumjali mjane wa Mohbad na mwanawe hata baada ya kifo chake.

Kwa vitendo vyao vya upendo, huruma, na mshikamano, Iyabo Ojo na binti yake Priscilla wanaendelea kuiheshimu kumbukumbu ya Mohbad na ukaribu unaokua kati ya Liam na Rakeem ni uthibitisho kwamba upendo wa kweli hauishi, bali huendelea hata baada ya maumivu ya kupoteza mtu muhimu kwako.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button