Ligi KuuNyumbani

Polisi Tanzania kunyoa au kusuka leo

LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea leo kwa mchezo mmoja mkoani Kilimanjaro.

Polisi Tanzania inayosuasua itakuwa mwenyeji wa Ihefu kwenye uwanja wa Ushirika mjini Moshi.

Maafande hao wanahitaji ushindi katika mchezo huo na michezo mingine inayofuata ili kuepuka kushuka daraja.

Ihefu inashika nafasi 8 katika msimamu wa ligi ikiwa na pointi 30 baada ya michezo 26 wakati Polisi ni ya mwisho nafasi ya 16 ikiwa pointi 19.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button