EPLKwingineko

Pochettino akaribia kutua Chelsea

KLABU ya Chelsea ‘The Blues’imekubaliana kimsingi na wawakilishi wa Mauricio Pochettino kwa ajili ya Muargentina huyo kuwa kocha wake mkuu mpya.

The Blues imekuwa ikisaka kocha wa kudumu kuchukua nafasi ya Graham Potter aliyetimuliwa kazi mwezi uliopita na imekuwa na mazungumza na makocha kadhaa kuhusu suala hilo.

Wamiliki wa Chelsea, Todd Boehly and Clearlake Capital kwanza walizungumza na mkocha wa zamani wa Barcelona Luis Enrique na Bayern Munich Julian Nagelsmann kuhusu nafasi hiyo.

Hata hivyo, Chelsea iliachana na Enrique baada ya mazungumzo ya awali huku Nagelsmann akijitoa kwenye mpango huo wiki iliyopita.

Related Articles

Back to top button