Kwingineko

Real vs City robo fainali UCL

BINGWA mtetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL)Manchester City itaikabili Real Madrid katika robo fainali ya michuano hiyo.

Katika droo iliyofanyika Nyon, Uswisi leo Arsenal itaivaa Bayern Munich wakati Barcelona itakiwasha dhidi ya Paris Saint-German.

Robo fainali nyingine itashuhudia Atletico Madrid ikikutana na Borussia Dortmund.

Michezo ya kwanza ya robo fainali hizo itafanyika kati ya Aprili 9 na 10 huku marudiano yakifanyika kati ya Aprili 16 na 17.

Nusu fainali za kwanza zimepangwa kupigwa kati ya Aprili 30 na Mei 1 wakati marudiano ni kati ya Mei 7 na 8.

Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itafanyika uwanja wa Wembley, London Juni 1, 2024.

Related Articles

Back to top button