Pluto: Sijamuona mwanangu Zoey mwaka sasa

NAIROBI: THEE Pluto amesema kwamba amekuwa katika hali ngumu kutokana na kutopata fursa ya kuonana na kuzungumza na mwanawe Zoey kwa karibu mwaka mmoja sasa.
Akizungumza kwenye kipindi cha Oga Obinna, Pluto alisema anaimani wataonana tu kwa kuwa hawakuwa na mawasiliano tangu Desemba 17, 2024.
Aidha, Pluto amesema suala hilo anajitahidi kulishughulikia kwa utaratibu na upore kwa sababu lilipofikia ni baya kwake.
Akizungumzia hali ya Zoey, Thee Pluto alisema, “Zoey, naamini yuko sawa. Kwa sababu hatuna mawasiliano kati yetu, tangu Desemba 17 mwaka jana.”
Pluto alieleza kuwa ukosefu wa mawasiliano umemfanya ahisi kukosa msaada kwa sababu hajui kinachoendelea katika maisha yake.
Pluto pia aliongeza kwamba kwa sasa hajamtumia fedha mwanawe kwa sababu anahisi si jambo la lazima kwa hali ilivyo. Alisema watu kwenye mitandao ya kijamii mara nyingi wanahukumu uhusiano wake na mtoto wake bila kuelewa kinachoendelea kwake.
Alisema, “Hii issue ni ngumu sana. Wakati mwingine, mimi hujiuliza, watu hawa wanaokuja kwenye sehemu ya maoni na kuanza kusema kila unachofanya ni sawa au si sawa. Labda watu hawa hawawezi kusema kwamba Zoey anahitaji baba yake.”
Mnamo Novemba 4, 2025, Thee Pluto aliandika ujumbe wa moyo mkunjufu akimtakia binti yake heri ya siku ya kuzaliwa: “Heri ya siku ya kuzaliwa, binti yangu Zoey. Natumai unaendelea vizuri. Nakutakia ufanikiwe na Mungu akupe baraka na kulinda. Natumai siku moja tutarudi pamoja.”




