Kwingineko

Guardiola alishiriki kuiangamiza Madrid

MADRID, Meneja wa Washika mitutu wa jiji la London Arsenal Mikel Arteta amemshukuru meneja wa Manchester City Pep Guardiola kwa kumhamasisha kuwaondosha Mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya Real Madrid kwa kuwafuga mabao mawili kwa moja nyumbani Bernabeu na kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.

Mhispania huyo alisifu kiwango cha wachezaji wake na kusema kuwa usiku huo ulikuwa usiku bora sana kwenye maisha yake huku akifichua kuwa alizungumza kwa simu Pep asubuhi simu iliyomhamasisha kufanya makubwa Bernabeu.

“Nilimpigia (Pep) asubuhi kwa sababu nimefika hapa kwa kwa sababu yake, kwenye mafanikio yangu ana mchango mkubwa sana, amekuwa mfano kwangu, nimekuwa chini yake kwa miaka minne bora sana nisingefika nilipo bila mchango wake” amesema Arteta

Arteta amewahi kufanya kazi chini ya Pep Guardiola kama kocha msaidizi wa Manchester City kuanzia 2016 mpaka 2019 alipoteuliwa kuwa meneja wa Arsenal na tangu awasili kikosini hapo anakiongoza kwa mara ya kwanza kwenye nusu fainali ya michuano hiyo yenye hadhi ya juu zaidi barani ulaya

Nyota ya Arsenal ilianza kuwaka katika dimba Emirates katika mchezo wa mzunguko wa kwanza walipowabugiza Real Madrid 3-0 kabla ya kushinda tena 2-1 Santiago Bernabeu na kuwaondosha kwa jumla ya mabao 5-1.

Related Articles

Back to top button