Nyumbani
Pamba yaifuata Pan African na matumaini kibao

TIMU ya Pamba ya Mwanza inaondoka leo kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa ligi ya Championship dhidi ya Pan African kwenye Uwanja wa Uhuru.
Akizungumza na gazeti la HabariLEO kabla ya kuanza safari, kocha msaidizi wa Pamba, Godfrey Chappa amesema timu yao ipo tayari kwa mchezo huo Machi 4, 2023.
“Timu yetu imepumzika vya kutosha tumetumia wiki moja kujiandaa dhidi ya
Pan African, tunatarajia mchezo kuwa mgumu ila sisi tutapambana kushinda,”
amesema Chappa.
Baada ya mchezo dhidi ya Pan African, Pamba itacheza na Transit Camp Machi
12 katika uwanja huo huo wa Uhuru kabla ya kumenyana na Green Warriors Machi 26 kwenye Uwanja wa Meja Isamuhyo.