World Cup
		
	
	
Nusu fainali Kombe la dunia wanawake leo

NUSU fainali ya kwanza ya Kombe la Dunia kwa wanawake kati ya Hispania na Sweden inapigwa leo jijini Auckland, New Zealand.
Mchezo huo utafanyika kwenye uwanja wa Eden Park ukiamuliwa na mwamuzi Edina Alves Batista wa Brazil.
Nusu fainali ya pili itakayozikutanisha Australia na England itapigwa Agosti 16 jijini Sydney, Australia.
				
					



