Nigeria pungufu yalazimisha suluhu Kombe la Dunia wanawake
						WAWAKILISHI wa Afrika katika fainali za Kombe la Dunia 2023 kwa wanawake, Nigeria leo imeanza kampeni ya michuano hiyo kwa kutoka suluhu na Canada licha kucheza pungufu dakika za mwisho baada ya Deborah Abiodun kutolewa kwa kadi nyekundu.
Mchezo huo wa kundi B umefanyika uwanja wa Melbourne Rectangular nchini Australia ukichezeshwa na mwamuzi Lina Lehtovaara wa Finland.
Timu nyingine ya Afrika, Zambia itaingia dimbani Julai 22 kuikabili Japan katika mchezo wa kundi C.
Katika mchezo mwingine wa kundi A leo Uswisi imeitandika Philippines magoli 2-0 kwenye uwanja wa Dunedin yakifungwa na Ramona Bachmann kwa penalti dakika ya 45 na Seraina Piubel dakika 64.
Mchezo huo umefanyika uwanja wa Dunedin, New Zealand ukichezeshwa na mwamuzi
Vincentia Amedome wa Togo.
				
					



