Nicki Minaj: Jay-Z lipa deni lako la dola milioni 200

NEW YORK: RAPA maarufu, Onika Tanya maarufu Nicki Minaj amemtaka msanii mwenzake ambaye pia ni bilionea katika muziki, Shawn Carter maarufu Jay-Z kuhusu madai ya deni lake analomdai.
Hitmaker huyo wa ‘Anaconda’ alidai kuwa bosi huyo wa Roc Nation anadaiwa takribani dola milioni 200.
Minaj alimsihi Jay Z amfikie na kumalizia deni hilo, akionya kwamba kutofanya hivyo kungesababisha riba zaidi.
Kwenye ukurasa weake wa X, Minaj ameandika, “Tumehesabu takriban 100-200ml kufikia sasa. #JayZ nipigie ili kumalizia deni hili la karmic. Inakusanya riba zaidi. Bado uko kwenye Top 5 yangu. Let’s get it nigga.”
Nicki Minaj amekuwa akimpigia simu Jay-Z, akidai alimlaghai kwenye malipo ya Tidal equity baada ya mauzo yake mwaka 2021.
Jay-Z bado hajajibu tuhuma za hivi punde za Nicki Minaj, nini kitaendelea usiache kufuatilia SpotiLeo kwa taarifa zaidi.