FANyumbani

Ni Yanga vs Kurugenzi, Simba vs Eagle ASFC

DROO ya pili ya mechi 64 Kombe la Shirikisho la Azam(ASFC) imefanyika leo huku miamba ya soka Yanga ikipewa Kurugenzi, Simba ikiiwinda Eagle na Azam kuonja Malimao.

Kwa mujibu wa droo hiyo mechi hizo zitaanza Desemba 9.

Michezo mingine itakuwa Mtibwa Sugar vs TRA Kilimanjaro, Tanzania Prisons vs Misitu, Singida Big Stars vs Lipuli, Coastal Union vs Tanga Middle na KMC vs Tunduru Korosho.

Mingine ni Fountain Gate vs Rhino Rangers, JKT Tanzania vs Biashara United, Ndunguti Stars vs Gwambina, African Lyon vs Mbuni, Kigoma Kwanza vs Buhaya, Cosmopolitan vs Mbeya Kwanza, Majimaji vs Ken Gold na Mashujaa vs Pamba.

Droo hiyo inaonesha mechi nyingine ni Polisi Katavi vs Mbeya Road, Mbao vs Mapinduzi, Green Warriors vs Stand United, Silent Ocean vs Copco, Magereza Dar es Salaam vs Pan African, E4M vs New Dundee, Afya vs African Sports na Nzega United vs KFC.

Mechi nyingine katika droo hiyo ni Geita Gold vs Transit Camp, Ihefu vs Mtama Boys, Kagera Sugar vs Buhare, Dodoma Jiji vs TMA, Ruvu Shooting vs Ndanda, Namungo vs Kitayosce, Polisi Tanzania vs Nyika na Mbeya City vs Stand.

 

Related Articles

Back to top button