Ned Nwoko: Sitaki kumuona Regina Daniels nyumbani kwangu

DELTA NORTH: MBUNGE anayeiwakilisha jimbo la Delta North, Ned Nwoko amekanusha madai kwamba anataka kurejea na mke wake wa zamani ambaye ni muigizaji wa Nollywood, Regina Daniels.
Hii imekuja baada ya Regina kudai kuwa seneta huyo alikuwa amewatuma wanachama wa familia yake kuomba msamaha kwa niaba yake.
Muigizaji mwenzake, Doris Ogala, pia aliunga mkono madai hayo kwa kupost kwenye Instagram, akisema kuwa Regina anachokifanya ni cha kweli.
Hata hivyo, Ned Nwoko, kupitia kwa kiongozi wake wa mawasiliano, amekanusha kabisa hadithi ya kurejea kwa Regina, na kusema hana mpango wa kumrudisha nyumbani kwake.
Seneta huyo pia alikana madai ya Regina kuhusu matumizi ya dawa za kulevya na tabia ya kufanya mambo ya kijinsia yasiyokubalika, akisema madai hayo ni uongo na hayana ushahidi wowote wa kuthibitishwa.
Nwoko alieleza kuwa matamshi ya Regina kwenye mitandao ya kijamii hivi karibuni ni matokeo ya “ushawishi wa dawa za kulevya” zinazomtesa.
Alisema kwamba mazungumzo yao ya mwisho kwenye WhatsApp yalikuwa na hisia za hasira kutoka kwake kuhusu tabia yake, na alimtaka Regina arudi kwenye matibabu kuachana na dawa hizo au atakapoteza msaada wa kifedha wa maisha yake.




