Tetesi

Napoli, Galatasaray kukubaliana dili la Osimhen

ITALIA: TIMU za Napoli na Galatasaray kwa sasa zipo katika harakati za kusaini na kubadilishana hati zinazohitajika kukamilisha uhamisho wa kudumu wa mchezaji wa kimataifa wa Nigeria, Victor Osimhen.

Kulingana na wataalamu wa taarifa za uhamisho Fabrizio Romano na Yağız Sabuncuoğlu, shughuli hiyo sasa iko katika ‘hatua ya kusaini’, huku mawakili wa vilabu vyote viwili wakifanya kazi ya kukamilisha uhamisho huo kabla ya mwisho wa wikendi.

Mafanikio hayo yalikuja mapema wiki hii wakati Napoli na Galatasaray walipofikia makubaliano madhubuti juu ya muundo wa malipo ya uhamisho wa Osimhen wa euro 75milioni.

Ingawa Galatasaray ilikuwa tayari kulipa bei kamili inayotakiwa, pande zote mbili ziliendelea na mazungumzo kuhusu masharti ya malipo, awamu na dhamana kabla ya kusuluhisha makubaliano yaliyopangwa.

Galatasaray italipa Napoli kiasi cha Euro milioni 75 ifikapo mwisho wa 2026, huku Euro milioni 40 zikilipwa mapema na zile milioni 35 zilizosalia kwa awamu hadi mwisho wa mwaka ujao.

Partenopei pia itakuwa na haki ya hadi Euro milioni 5 katika bonasi na itahifadhi kifungu cha mauzo cha asilimia 10 katika makubaliano.

Osimhen ataondoka Napoli baada ya miaka mitano kwenye vitabu vya klabu hiyo, huku msimu wa mwisho akiwa kwa mkopo Istanbul akiwa na Galatasaray.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Nigeria alifunga mabao 65 ya Serie A katika mechi 108 za ligi wakati alipokuwa Naples na alipokuwa Capocannoniere Napoli ikishinda taji lao la kwanza la Serie A tangu enzi ya Diego Maradona msimu wa 2022/23.

Muda wake wa mkopo na Galatasaray 2024/25 ulileta hali ya kutisha mbele ya lango, akiwa na mabao 37 alifunga na kutoa asisti nane kutokana na mechi 41 katika michuano yote.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button