Mwinyi atembelea mjusi wa Tendaguru

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi leo ametembelea mabaki ya mjusi mkubwa (Dinosaur) wa Tanzania aliyeko Berlin, Ujerumani.
Mjusi huyo anayehifadhiwa katika makumbusho ya Fuer Naturkunde alingundulika katika Kijiji cha Tendaguru Mkoani Lindi, Tanzania mwaka 1906/07.
Taarifa ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imesema Dkt. Mwinyi pia ametembelea ukuta wa Berlin uliojengwa na Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Ujerumani Agosti 1961 na kudumu hadi Novemba 1989, kwa lengo la kuzuia raia wa mashariki ya Ujerumani kutoroka kwenda Magharibi.
Katika msafara huyo Rais Dk. Mwinyi ameambatana na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Balozi Dk. Pindi Chana, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar Tabia Maulid Mwita, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Dk Abdallah Saleh Possi.