Kwingineko

Neymar kwenda Chelsea?

FOWADI wa Paris Saint-Germain, Neymar da Silva Santos Júnior, maarufu Neymar Júnior, huenda anaelekea Chelsea ‘The Blues’ baada ya washauri wake kuripotiwa kuendelea kufanya mazungumzo na The Blues kuhusu uwezekano wa uhamisho.

Neymar amewaambia mabingwa wa Ligue 1 anataka kuondoka majira haya ya joto na anakuwa nyota wa hivi karibuni kuipa kitendawili kingine timu hiyo huku hatma ya Kylian Mbappe haijatatuliwa.

Nyota huyo wa Brazil alijiunga na PSG katika uhamisho uliovunja rekodi mwaka 2017 wa ada ya pauni milioni 198 sawa na shilingi bilioni 607.46 toka Barcelona na sasa ana nia kukamilisha dili kabla ya dirisha la uhamisho ulaya ufungwa.

Neymar amebakisha miaka miwili katika mkataba wake wa sasa PSG ukiwa na chaguo la kuongeza mwaka mmoja zaidi baada ya kuongeza mkataba mpya 2021.

Kulikuwa na mazungumzo wakati wa dili hilo kwamba Neymar mwenye umri wa miaka 31 alikuwa aking’ng’ania uhamisho kurejea Barcelona kabla ya kusaini dili lenye thamani ya pauni milioni 26 kwa mwaka.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button