Mwanamke China atoa burudani ya mwaka

CHANG SHA: MWANAMKE mmoja nchini China aliamua kumtangaza rafiki yake na mpenzi wake kwa mabango hadharani baada ya kuwafuma wakiwa katika mahusiano ya kimapenzi.
Mwanamke huyo aliandika katika mabango hayo mambo ya kuwadhalilisha akiwatuhumu kuwa na uhusiano kwa zaidia ya miaka m itano bila yeye kujua.
Mwanamke huyo alitundika mabango hayo makubwa kwenye uzio wa makazi huko Changsha, mkoa wa Hunan na kumshukuru kwa kejeli rafiki yake , aitwaye Shi, kwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mumewe.
Hakutumia tu mabango kufichua uchumba wa mume wake na rafiki yake huyo lakini pia alieleza kwamba Shi, rafiki yake wa miaka 12, anafanya kazi katika idara ya fedha ya ofisi ya usimamizi wa utalii katika jumuiya ya Hongshan.
Mojawapo ya mabango hayo yalisomeka, “Shi anakiuka utaratibu wa umma na maadili mema, kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mume wa rafiki yake na kujiita “Mke.”
“Asante Kwa Kulala na Mume Wangu”aliandika mwanamke huyo.




