Filamu

Muongozaji filamu awakataa Salman Khan, Madhuri Dixit

MUMBAI: MUONGOZAJI wa filamu Sooraj amesema katika filamu yake anapenda kuwatumia waigizaji chipukizi badala ya kuwatumia Salman Khan wala Madhuri Dixit sababu ya umri wao mkubwa.

Katika mazungumzo na Times of India, Sooraj amesema hatamtaka Salman Khan wala Madhuri Dixit katika safu inayofuata ya ‘Hum Apke Hain Koun’.

Akielezea sababu zake, Sooraj amesema, baada ya kufikia umri fulani, mara nyingi watu huamini filamu nzuri kuliko nyota.

Muongozaji huyo ambeye pia ni muigizaji ameeleza kuhusu uhusiano wake na Salman Khan, lakini akasema ikiwa tu kutakuwa na hadithi yenye wahusika wanaomfuata yeye na Madhuri, ndipo atakapotaka kufanya kazi na nyota hao tena. “Siku zote nimeamini kuwa hati nzuri ni kubwa kuliko kitu kingine chochote.”

Hapo awali, akizungumza kuhusu Salman Khan, Sooraj aliiambia Mid-Day, “Siku zote aliamini kwamba filamu ilikuwa muhimu zaidi, na bado iko leo. Hata sasa, kama ninataka kutengeneza filamu na mtu mwingine, angeniunga mkono, na hata kuuliza kama nilimhitaji kufanya maonesho ya wageni.

Sooraj ameongeza kuwa kwa sasa wasanii hao umri wao umeenda hivyo kama atawashirikisha katika filamu zake itachukua muda kwani lazima hadithi ziwe za kuendana na umri wao.

Related Articles

Back to top button