Filamu
Muigizaji wa filamu Radhakrishnan Chakyat amefariki dunia

MUMBAI: MUIGIZAJI na mpiga picha mashuhuri wa Kimalayalam, Radhakrishnan Chakyat amefariki dunia kutokana na mshtuko wa moyo akiwa na miaka 53.
Katika taarifa iliyotolewa na Dulquer Salmaan juu ya kifo cha muigizaji huyo inaeleza kuwa amefariki Mei 22 akiwa na umri wa miaka 53.
Radhakrishnan Chakyat alianza kazi yake ya kusaidia mpiga picha maarufu wa mitindo Rafique Sayed huko Mumbai.
Baada ya kujifunza upigaji wa picha kwa muda mrefu aliamua kuwa wakala wa matangazo na akawa mpiga picha wa kujitegemea.
Kwa miaka mingi, alishirikiana na wanamitindo na chapa bora kama vile Cadbury, Hoteli za Taj, Rangi za Asia, Corelle, na Roca na nyingine nyingi. Kazi yake ilijizolea umaarufu kihisia, ustadi na kiufundi.