
CHENNAI: MUIGIZAJI wa Kitamil ambaye ni Mwalimu wa Karate, Shihan Hussaini amefariki dunia kwa saratani ya damu huko Chennai nchini India.
Familia ya muigizaji huyo iliweka wazi jana kupitia ukurasa wake wa Facebook, wanafamilia hao wamesema kwamba mabaki yake yatahifadhiwa katika makazi yake ya Besant Nagar hadi jioni.
Kwa mujibu wa familia yake mwili wa Shihan umetolewa kwa ajili ya utafiti wa kimatibabu. Muigizaji huyo amecheza filamu kama vile ‘Punnagai Mannan’ na ‘Kaathu Vaakula Rendu Kaadhal’.
Chapisho hilo lilisomeka, “Nina huzuni sana kukutaarifu kwamba Hu ametuacha. Hu atakuwa kwenye Amri Kuu, makazi yake huko Besant Nagar hadi jioni. Hussaini na familia, Kamana/Mahima.”
Pia wanafamilia hao waliandika chapisho linguine lililoeleza: “Wapenzi wapiga mishale, wazazi, na makocha, Yeyote anayekuja nyumbani kwa HU kuona mabaki yake ya kufa, tafadhali njoo ukiwa na sare yako (rangi yoyote ni nzuri), na ikiwezekana, njoo na upinde na mshale wako ili kurusha mishale michache,
“Mabaki yake ya kufa yatakuwa katika amri ya juu hadi saa 7 mchana. Wapiga mishale wote watapiga mishale michache saa tano ambapo Hu atakuwa akisimamia risasi kupitia mwili wake. Karateka zote, watacheza saa tatu usiku watafanya kata ya mapigano mbalimbali kama ishara ya kumuaga muigizaji huyo,” walieleza familia yake wakitoa ratiba ya matukio itakavyokuwa katika msiba wa muigizaji huyo.