
LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea leo kwa michezo mitatu, kivutio kikiwa msako wa nafasi ya pili unaohusisha Simba na Azam.
Azam inayoshika nafasi ya pili katika msimamo ikiwa pointi 60 baada ya michezo 27 itakuwa mgeni wa JKT Tanzania iliyopo nafasi ya 9 ikiwa na pointi 31 kwenye uwanja wa Isamuhyo, uliopo Mbweni, Dar es Salaam.
Simba iliyopo nafasi ya tatu ikiwa na pia na pointi 60 baada ya michezo 27 itakuwa mwenyeji wa Geita Gold inayoshika nafasi ya 15 ikiwa na pointi 25 kwewye uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.