Nyumbani

Msuva :Tunapambania Taifa dhidi ya Morocco

TANGA: Mshambuliaji wa timu ya Taifa Stars, Simon Msuva, amesema kikosi hicho kinatakiwa kupambana kwa ajili ya taifa katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Morocco utakaochezwa Machi 26, katika mji wa Oujda, Morocco.

Msuva amekiri kuwa mchezo huo hautakuwa rahisi kutokana na ubora wa Morocco, timu yenye wachezaji wanaocheza katika ligi za Ulaya na Asia.

“Kama wachezaji tumejiandaa kukabiliana nao. Benchi la ufundi limefanya kazi kubwa kwa kuchambua madhaifu yao na kutengeneza mbinu sahihi za kukabiliana nao,” amesema Msuva.

Ameongeza kuwa wanaelewa changamoto ya kucheza ugenini, lakini wamejiandaa kwa mbinu tofauti zitakazosaidia kupambana na wenyeji hao.

“Kikubwa ni kuomba uzima na afya njema. Tunaamini wachezaji wote waliopo kambini wanajituma ili kuhakikisha tunapata matokeo mazuri kwa heshima ya taifa letu,” amesema Msuva.

Taifa Stars, chini ya kocha Hemed Morocco, imeweka kambi jijini Tanga kwa maandalizi ya mchezo huo kabla ya kusafiri kuelekea Morocco kwa ajili ya pambano hilo muhimu.

Related Articles

Back to top button